Sunday, October 21, 2012


Wakuu wa Misri wanasema kuwa wamezuwia mali ya waziri mkuu wa mwisho wa utawala wa Rais Hosni Mubarak.


Mwanasiasa huyo ni Ahmed Shafiq ambaye alishindwa kwa kura chache na Mohammed Morsi kwenye uchaguzi wa rais mwezi wa Juni. Msemaji wa wizara ya sheria ya Misri alisema kuwa wanachunguza tuhuma kwamba Bwana Shafiq alipata mali yake nyingi kwa njia zisokuwa halali, pamoja na nyumba 12 na fleti mbili. Bwana Shafiq, ambaye hivi sasa yuko katika Falme za Kiarabu, amekanusha tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment

Tupatie maoni yako sasa!