CHAT FLOW

chat room

5 comments:

  1. Viongozi wamezidi pere pere nyingi utedaji wa kazi f

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo ni kwamba viongozi hufanya siasa kama biashara

      Delete
  2. Jamani vijana wenzangu! Hebu tuungane tulete mabadiliko Ndungu, vijana weng wanaharibika kwa pombe na bhangi, vilevile tupige kelele kuhusu barabara, kwani toka madaraja yavunjwe na maji hayakurekebishwa, mfano hili lilopo kwa mzee seif mpaka leo nadhan bado, inamaana mvua ikinyesha usafiri utakua wa tabu. Tunahitaji ijengwe ktk kiwango cha lami ili ipitike season zote, na endapo ikiwekwa lami basi hata maendeleo yatakua kwa kasi ukilinganisha na sasa..Sisi ndiwo wakuibadili ndungu, TUSIMAME KWAPAMOJA TUNAWEZA

    ReplyDelete
  3. Habari wana NDUNGU
    Nina maoni tofauti lkn ya kimaendeleo,
    Nimejaribu kuangalia jinsi kilimo cha mpunga kinavyoendeshwa hasa ukizingatia gharama zake,muda,processing time na hadi kutafuta soko la mchele.

    Kwa maoni yangu ukiangalia economic positive side naona kama bado sio kilimo hasa cha biashara na si profitable kiasi cha kumfanya mkulima akivuna asiwe na wasi wasi hata asipolima msimu unaofuata.

    Kwa mfano hebu angalia kipindi baada ya kuvuna hadi kuuza halafu kipindi cha kuandaa shamba,kutuliza,kipindi chote hiki anatumia nini anakula nini nikiwa na maana matumizi yake yanatoka wapi kama sio katika yale mavuno yaliyopita ?

    Na inawezekana pia asiweze kumudu baadhi ya gharama za ukulima inabidi akope mbolea,pesa ya kumwagilia maboda maji (water charges) na mambo mbalimbali yahusuyo shamba zima na kilimo kwa ujumla.

    Nahisi bado kilimo hiki hakijawakwamua watu wetu kwa maana ya kukuza uchumi wao na kuwafanya wawekeze katika shughli nyingine kutokana na kipato cha kilimo hiki.

    Hii ni tofauti sana na maeneo mengine katika Tanzania yetu ambapo kilimo kama cha Nyanya kule Iringa, Mananasi kule Pwani (bagamoyo), mahindi Iringa,mpunga Kyela,viazi mbatata Iringa na Mbeya na kadhalika.

    Juhudi za pamoja zinahitajika kufanya research ya nguvu katika kilimo hiki cha mpunga hapa kwetu Ndungu wakati huo huo ukilinganisha hali za kiuchumi za wakaazi wetu ambao bado wanaendelea kulima zao hili kwa toka miaka ya mwishoni mwa tisini hadi sasa bila kujikwamua kiuchumi kwa maana halisi ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hata jamii (kijiji) kwa ujumla.

    Ni mimi,
    RAMADHAN J.HUSSEIN
    DSM (kwa sasa niko Tanga)

    Ni mzaliwa toka kwa mama BAHATI (marehemu)wa hapo Turiani,
    Kwa kifupi ni mtu wa ukoo wa Mirambo WAMBELE (Mjomba wangu)

    ReplyDelete

Tupatie maoni yako sasa!