NDUNGU LOCATION

ndungu location

Ndungu location


Ndungu ni jina la kata iliyopo Wilayani Same katika Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata hiyo ina wakazi wapatao 14,044 waishio humo.


Wenyeji wa kijiji hicho ni wa kabila la Kipare ambao hushughulika sana na kilimo cha mpunga

kijiji cha ndungu kipo karibu na hifadh ya wanyama ya mkomazi

Hifadhi ya Mkomazi ipo katika mikoa miwili ambayo ni Kilimanjaro na Tanga, ndani ya wilaya za Same na Lushoto nchini Tanzania. Hifadhi ya Mkomazi ilianzishwa mnamo mwaka 1951 kama Pori la Akiba lilitengwa kutoka katika Pori kubwa la Akiba la Ruvu. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 3245 (Kilometa za mraba 2010.4 ni Mkomazi na Kilometa za mraba 1224.1 ni Umba).

Pori hili lilipendekezwa kuwa hifadhi ya taifa kwa misingi ya kunusuru maeneo na rasilimali zilizomo kutokana na matumizi yasiyoendana na uhifadhi kwa ajili ya kizazi cha leo na kijacho. katika hifadhi hii kuna wanyama na ndege wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbwa pori na vifaru weusi walioingizwa kutoka kutoka nchi ya Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment

Tupatie maoni yako sasa!