Sunday, October 21, 2012


Duru za jeshi la Guinea Bissau, Afrika Magharibi, zinaeleza kuwa watu waliokuwa na silaha wameuwawa kwenye shambulio dhidi ya kambi ya jeshi nje ya mji mkuu, Bissau.


Inaarifiwa mapambano yaliendelea kwa saa nzima. Waandishi wa habari wanasema shambulio hilo lilofanywa usiku wa manane, litazidisha wasiwasi Guinea Bissau, ambako jeshi lilipindua serikali mwezi wa Aprili. Fujo za mara-kwa-mara nchini Guinea Bissau zimeifanya nchi hiyo kuwa pahala pa kupitisha magendo ya mihadarati, baina ya Amerika Kusini na Ulaya.

No comments:

Post a Comment

Tupatie maoni yako sasa!