Friday, September 16, 2016

NUFAIKA NA BENK ZA TANZANIA

http://crdbbank.com/

Thursday, September 15, 2016

FUNITURE Warehouse Ltd

DISCOUNT KABAMBEE.!!

BET-Africa

Do your friends like your partner? Steph tries to get Kamie and Kevin to hash things out but things get out of hand when Eny intervenes. Catch the  #FinFabulous drama tonight @ 21:50 CAT.

KUMSAIDIA MKEO KAZI ZA NYUMBANI JE NIKUKALIWA AU NI MAPENZ YA DHATI?

Coca-cola

BREAKING NEWS: Trey Songz ategemewa kupiga show Coke Studio Africa October hii! Vionjo vyote vya msimu wa nne wa Coke Studio Africa hivi hapa http://spr.ly/6187BAstU

Whitedent Tanzania

Gari letu la maonesho  wiki hii litakua maeneo yafuatayo. Tafadhali ungana nasi kwa kwenda kujaza fomu katika sehemu hizi husika ili uweze kuwa mmoja wa mshindi wa magari 25 kutoka whitedent. Karibu sana!

Gari no 1 Kinondoni 1 - Mtaa: manzese daraja
Gari no 2 Kinondoni 2 - Mtaa : Ubungo River side
Gari no 4 Ilala               - Mtaa : Buguruni Sheli
Gari no 7 Arusha          - Mtaa :Kirombelo bus stand
Gari no 10 Zanzibar     - Mtaa : Mkunazini Unguja
Gari no 12 Mbeya         - Mtaa : kabwe mbeya
Gari no 15 Songea       - Mtaa :Machine ya mpunga (manzese)
Gari no 17 Singida       - Mtaa :Msifuni Sokoni
Gari no 18 Tabora        - Mtaa :Tabora Stand Mpya
Gari no 19 kigoma       - Mtaa :Soko la mwanga
Gari no 24 Geita           - Mtaa : nyankumbu

Wakumbuka hili shairi

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI"

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake, nasisitiza, kama mnataka mali mtaipata shambani

JINS YAKUONDOA WEUSI KWENYE MAKWAPA

Njia 3 Asili za Kuondoa Weusi katika Makwapa na Mapaja  Inner thighs/mapaja ya ndani na makwapa hutokea weusi kutokana na msuguano wa ngozi kwasababu ya mapaja kugusana, hata ngozi iliyokauka pia inaleta weusi katika ngozi. Hivyo nimekuletea njia natural ya kuondoa weusi huo bila kutumia madawa makali.  1.TUMIA MAFUTA YA NAZI NA NDIMU. Mafuta ya nazi yanatumikakulainisha ngozi lakini unaweza kutumia pia katika kuondoa weusi ukichanyanya na ndimu.. Fata step hizi:: Chukua vijiko 3 vya mafuta ya nazi changanya na ndimu nusu Paka sehemu yenye weusi katika mapaja huku ukisugua kama unafanya massage kwa dakika 15. Kisha osha na maji ya uvuguvugu na kausha kwa kitambaa kilaini na kisafi.  2.TUMIA MCHANGANYIKO WA SUKARI ASALI NA NDIMU. Mchanganyiko huu pia unaweza ukaondoa weusi katika mapaja na makwapa, fuata step hizi:: Changanya kijiko kimoja cha asali, ndimu nusu na kijiko kimoja cha sukari. Paka sehemu yenye weusi na sugua kawaida hadi sukari ipotee. Acha ikae kama dakika 10 kisha osha na maji ya uvuguvugu.  3.GANDA LA CHUNGWA NA ASALI Kama mnavyojua machungwa yana vitamin C, na hivyo ukichukua ganda la chungwa pamoja na asali, mchanganyiko wake pia unaondoa weusi. Fuata step hizi:: Chukua ganda la chungwa na kijiko kimoja cha asali. Kamua hilo ganda maji yake yangie kwenye asali. Kausha nakusaga hilo ganda kisha poda yake ichanganye na asali Paka mchanganyiko huo katika sehemu yenye weusi, kaa kwa muda wa dakika 15 Osha na maji ya kawaida hadi kugandaganda kupotee.

Mobile tracking

Detect Any Mobile Number Location Using This This Application for android... simple and easy to download no survery goto : http://ft7.in/Mobile_Number_Tracker

Wednesday, September 14, 2016

HILI SWALA LINA UKWELI?

JE UNANDOTO ZAKUMILII NYUMBA ? INGIA HAAPA

http://kopabayport.co.tz/

WAZIRI MKUU NAE YUMO

Waziri Mkuu Majaliwa: aziagiza halmashauri zote nchini kutekeleza mpango kazi wa anwani za Makazi na Postikodi   Na Beatrice Lyimo na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma 14/09/2016 . Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameziagiza halmashauri zote nchini kutekeleza mpango kazi wa anwani za Makazi na Postikodi kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wananchi. Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo leo kabla ya kuzindua Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Mwongozo wa Postikodi uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa uliopo ndani ya viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma. “Nikizingatia hatua ambazo zimechukuliwa na Serikali katika kuweka mazingira ya utekelezaji wa anwani za makazi, naagiza halmashauri zote nchini kuzifanyia kazi changamoto ambazo hazihitaji fedha ama ambazo hazihitaji gharama kubwa” amesema Waziri Mkuu Majaliwa. Waziri Mkuu amebainisha baadhi ya changamoto ambazo hazihitaji gharama kuwa ni pamoja na kuhakikisha barabara na mitaa yote inakuwa na majina yaliyorasimishwa na wananchi wenyewe, kudhibiti mipango miji dhaifu na ujenzi holela, kuwa na takwimu za idadi ya barabara na mitaa na nyumba katika kila kata na kuwa na taarifa za wakazi katika kila kata. Changamoto nyingine zisizohitaji gharama kubwa ni kujengea uelewa wadau na wananchi kuujua na kuwa mfumo huo, kuimarisha matumizi ya daftari la wakazi ambapo taarifa za utekelezaji wa kazi hizo Waziri Mkuu ameagiza ziwasilishwe Ofisi ya Rais TAMISEMI kabla ama ifikapo mwezi Desemba, 2016. Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa kufuatia nia ya Serikali kuhamia Dodoma, manispaa ya Dodoma na halmashauri ya Chamwino zipewe kipaumbele cha utekelezaji ili kuweka mazingira mazuri ya kuishi na kufanya kazi. “Utekelezaji wa Mpango katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino ukamilike kabla ama ifikapo mwezi Desemba, 2016 na kuhakikisha utekelezaji huo kukamilika kwa wakati” amesema Waziri Mkuu Majaliwa. Kwa upande mwingine Waziri Mkuu amezitaka wizara za Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Manispaa ya Dodoma, Halmashauri ya Chamwino, CDA; TCRA na TPC zishirikiane ipasavyo katika kukamilisha mpango wa anwani katika mkoa huo. Mbali na hayo, Waziri Mkuu amezitaka taasisi za TANROADS, TBA, NHC, Mipango Mji na Mradi wa Kuboresha Miji (TSC) zinapoandaa mipango hususan mipango ya miundombinu na makazi, ziainishe pia anwani za makazi kwa kushirikiana na Halmashauri katika maeneo husika. Katika kufanikisha hilo, Waziri Mkuu amezitaka Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Wizara ya Unjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, TCRA na TPC kushiriki ipasavyo katika utekelezaji wa mpango hususan katika kujenga uelewa na uwezo kwa viongozi na watendaji wa halmashauri ili waweze kutekeleza mpango huo ipasavyo.  Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene amesema kuwa Mpango huo umefanyiwa majaribio katika majiji mawili ya Dar es salaam na Arusha pamoja na manispaa za Dodoma na Zanzibar. Waziri Simbachawene aliongeza kuwa ili kuwa na Tanzania ya kisasa, anwani za makazi ni kigezo muhimu cha kuzingatiwa katika kundeleza majiji, manispaa, halmashauri, kata na hata mitaa ambayo ndio inajenga taswira ya nchi

Kwa habari zaidi kuhusu waathirika wa tetemeko mwnza

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Mbatia-alilia-misaada-ya-waathirika-tetemeko/1597578-3381514-oke55u/index.html

Maisha ya ndoa yanahitaji kusaidiana

Sunday, November 4, 2012

MILA NA DESTURI ZA WAPARE


Wapare ni kabila kama yalivyo makabila mengine 120 nchi Tanzania na wanaishi kaskazini mwa Tanzania katika Mkoa wa kilimanjaro hasa katika wilaya za Mwanga na Same. Wilaya za Mwanga na Same ilikuwa moja ikijulikana kama wilaya ya Pare kabla ya kugawanywa na kuwa wilaya mbili yaani Same na Mwanga. wapare wamegawanyika katika sehemu mbili yaani kaskazini na kusini, upande wa kaskazini ipo wilaya ya Mwanga na Upande wa kusini ipo wilaya Same. kilugha pia wapare wamegawanyika; Wagweno wanaongea kigweno ambacho ni mchanganyiko wa Kichaga na kipare, na wapare wengine wanaongea Chasu, Kihistoria inaaminika kuwa asili ya wapare ni Kenya hasa kwenye miji ya Taveta na maeneo yote yanayouzunguka Mji huo. Neno Pare lina maana ya kuparua, kuondoa ngozi fulani au gome la mti, kwenye mti husika au kuparua samaki. Pia neno hili lina maana ya kifaa cha kuhifadhi aina fulani za vifaa kama vile visu na silaha nyingine. Kijografia Mji wa Mwanga unajihusisha sana kilimo na Mifugo. na sehemu nyingi ni milimani Milima ya Upare ni maarufu kwa ukulima wa Mahindi pamoja na mazao mengine ya chakula kama vile viazi, mihogo, Ndizi, Miwa n.k. Pia wanajihusisha na Ufugaji wa Ng'ombe mbuzi na Kondoo. Jamii ya kipare ni jamii mojawapo kati ya jamii chache za Tanzania ambazo zinatumia mfumo wa Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu, yaani wanafanya kazi kwa umoja na ushirikiano wa hali ya juu ili kujiletea maendeleo yao na ya taifa kwa ujumla. Kwa kutekeleza hayo jamii hii ya kipare imejiwekea utaratibu ambao unatumika ili kujiletea maendeleo, na utaratibu huo hujulikana kama Msaragambo. watu wote hutoka na kufanya kazi ya Pamoja eidha katika shamba la ushirika au pia kutengeneza barabara, mifereji ya maji, kujenga shule, Zahanati, na mambo mabalimbali kama hayo. Jamii nyingi za kipare pia zina utaratibu wa kushirikiana hata kwa mambo madogo madogo zaidi hasa kwa familia zilizo karibu karibu zaidi, kama vile kushirikiana katika chakula, kuchota maji pia wamama wana ushirikiano hasa kwa kusaidiana katika mambo ya familia kama vile kukata kuni n.k. Na inapotokea suala sherehe au misiba pia jamii hii hupenda kutoa ushirikiano mkubwa zaidi kwa mambo yote yanayo husiana na taratibu mbalimbali za msiba kulingana na mila na desturi za ukoo husika. Kabla ya kuendelea mbele hebu tuangalie koo zilizo katika jamii hii husika ya Wapare. Kuna zaidi ya koo 25 za wapare ndani ya milima ya upare lakini hapa nitataja baadhi tu ya koo hizo, wasuya washana wasangi wasoffe wawanga walacha wankeni wambaga wagonja wanzava wavamba wamamba washamba wadee n.k. Koo hizi na nyingine ndizo zinazounda kabila hili la kipare. Kwa ujumla hawa wote wanaishi maeneo hayo ya Upareni na pia wamesambaa katika tanzania nzima. Kama yalivyo makabila mengine ya tanzania Wapare wana watani wao ambao ni wachaga ambao pia ni wenyeji wa mkoa huo wa Kilimanjaro. Wapare ni kabila lenye uvumilivu kwa mambo mbalimbali zaidi hasa. ni kabila lisilo kata tamaa haraka zaidi. Kwa leo naishia hapa na baadaye nitaweza kuchambua zaidi juu ya MILA NA DESTURI ZA KILA KOO YA KIPARE.

Tuesday, October 23, 2012

MDAHALO WA KUGOMBEA URAISI


MAREKANI: MDAHALO WA MWISHO WA WAGOMBEA WA URAIS


Nani msema ukweli? Nani amewashawishi wapiga kura vya kutosha kabla ya uchaguzi? Ni Obama au Romney? Wagombea katika uchaguzi mkuu wa Marekani Barack Obama na Mit Romney wametofautiana kuhusu sera ya kigeni,Obama akisema Romney hana uelewa wowote wa sera ya kigeni wakati Romney akisema Obama alikosea katika sera yake ya Mashariki ya kati. Kwamba amesababisha vurugu zaidi tangu aingine mamlakani.

TAMKO LA RAISI!


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete , amesema serikali haitawavumilia waumin wachache wa madhehebu ya dini wanaotaka kuvuruga amani ya nchi kwa maslahi yao na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote wanaochochea uvunjivu wa amani.

Monday, October 22, 2012

MZOZO WA TANZANIA NA MALAWI


Rais Jakaya Kikwete anataka mahakama ya kimataifa kuhuzu mizozo kutatua mzozo kati ya nchi yake na Malawi



Hali ya wasiwasi inatanda kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mzozo wa mpakani ambao umekuwa ukitokota kwa miaka mingi lakini sasa umefika daraja ya juu katika wiki chache zilizopita.


Mzozo unahusu umiliki wa ziwa Malawi ambalo ni la tatu kwa ukubwa barani Afrika na ambalo linapakana na Malawi, Tanzania na Msumbiji.Tangu miaka ya sitini, Tanzania na malawi zimekuwa zikizozana kuhusu umiliki wa ziwa hilo, lakini mzozo huu wa sasa umekuwa mbaya zaidi hasa ikizingatiwa ripoti za kupatikana gesi na mafuta katika ziwa hilo..Msumbiji haijahusika kivyovyote na mzozo huu..


Nini hasa kinazozaniwa?


Fahari ya nchi na maswala ya kujiendeleza kiuchumi kwa Malawi na Tanzania kila mmoja akisimama kidete kusisitiza msimamo wake. Kwa Tanzania, ziwa hilo linajulikana kama Nyasa, wakati nchini Msumbiji inajulikana kama Lago Niassa. Malawi na Tanzania ni koloni za zamani za Uingereza wakati Msumbiji ilikuwa chini ya ukoloni wa Ureno. Uingereza iliichukua Tanzania kutoka kwa Wajerumani baada ya wao kushindwa katika vita vya kwanza vya dunia. Kando na ripoti za kuwepo mafuta na gesi katika ziwa hilo, ziwa lenyewe ni kivutio kikubwa cha watalii. Malawi inasema inashauriana na Msumbiji kuhusiana na uchimbaji wa mafuta katika siku za baadaye ili kuzuia mzozo wa kidiplomasia . Je hii ni mara ya kwanza kwa mzozo huu wa ziwa Malawi kutokea? Hapana. Mapema miaka ya sitini, Malawi ilidai umiliki wa ziwa hilo kwa kuambatana na makubaliano ya mwaka 1890 Heligoland kati ya Uingereza na Ujerumani ambayo yalisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo uko upande wa Tanzania. Makubaliano hayo yaliafikiwa na Muungano wa Afrika na Tanzania ikaitikia ingawa shingo upande. Mzozo mpya kati ya nchi hizo ukaripotiwa tena kati ya mwaka 1967 na 1968.

Kisiwa cha Likoma kwenye ziwa Malawi


Nini chanzo cha mzozo huu wa hivi sasa?


Mwezi Septemba mwaka 2011, Malawi ilitoa leseni ya kuchimba mafuta kwa kampuni ya British Surestream Petroleum Limited. Sehemu iliyotolewa kwa uchimbaji wa mafuta ni sehemu yenye mraba wa kilomita 20,000 sehemu ambayo Tanzania inasema ni yake. Vyombo va habari viliripoti mwezi Julai kuwa , mitumbwi ya wavuvi na ya watalii kutoka Malawi inavuka na kuingia upande wa Tanzania Tanzania nayo ikasema kuwa itatafuta ushauri kutoka jamii ya kimataifa ikiwa nchi hizo hazitaweza kusuluhisha mzozo huo zenyewe. Nchi hizo mbili zilifanya mkutano mwezi Julai mjini Dar es Salaam kuhusu mzozo wa mpaka Tarehe 30 mwezi Julai, Tanzania, iliitaka Malawi kusitisha shughuli za kutafuta mafuta kwenye ziwa hilo hadi mzozo kati yao utakaposuluhishwa lakini maafisa wa Malawi wakasisitiza kuwa ziwa hilo lote ni la Malawi na kwamba hakuna sababu ya kusitisha shughuli zake za kutafuta mafuta Tanzania ilisema kuwa ikiwa Malawi itaendelea na shughuli zake kutafuta mafuta itaathiri mazungumzo yanayoendelea kati ya nchi hizo mbili. Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe alisema kuwa ikiwa Malawi haitafuata maagizo hayo, Tanzania itaiona hatua yake kama kitendo cha uvamizi.

Rais Joyce Banda anataka Muungano wa Afrika kutatua mzozo wa ziwa Malawi


Nini kimesababisha hofu ya hatua za kijeshi?


Hofu ya mzozo kutokota na kuwa mbaya zaidi ilijitokeza wakati Tanzania iliposema kuwa italinda mipaka yake na kuzingatia sheria za kimataifa.Maafisa kutoka pande zote walikutana tena mjini Dar es tarehe 4 na 5 mwezi Agosti, lakini Malawi ilisisitiza kuwa haitasitisha shughuli zake za kutafuta mafuta Waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania Membe alinukuliwa akisema katika taarifa yake kali kuwa watapambana na Malawi kijeshi. Matamshi yake aliyatoa bungeni kulingana na taarifa kwenye mtandao wa The Guardian. Mtandao wa Nyasa Times ulitoa taarifa kuonyesha kuwa kuna taharuki kati ya nchi hizo mbili kuhusu mpaka wa Ziwa , lakini waziri wa usalama wa ndani wa Malawi Uladi Mussa akasisitiza utulivu. "Tunashauriana na serikali ya Tanzania na mambo yatakuwa sawa. Ikiwa hali itakuwa mbaya kesi hii tutaiwasilisha kwa mahakama ya kimataifa ya haki" alisema waziri huyo. Mnamo tarehe 11 mwezi Agosti, Rais wa Malawi Joyce Banda alisema kuwa yuko tayari kufanya kila hali ikiwemo kujitolea maisha yake kwa sababu ya watu wa Malawi. Watanzania wanaoishi karibu na ziwa hilo wakaanza kutoroka wakihofia vita. Je kumekuwa na juhudi za kidiplomasia kumaliza mzozo huu? Maafisa wa chi hizi mbili walikutana kati ya tarahe 20 na 25 mwezi Agosti, mjini Mzuzu,Kaskazini mwa Malawi, lakini Rais Banda akarejelea msimamo wake kuwa ni wazi kuwa Ziwa hilo ni la Malawi. Wakati wa mkutano wa chi za ukanda wa Afrika Kusini (SADC),nchini Msumbiji, Rais Banda alikutana na mwenzake wa Tanzania Jakaya Kikwete, aliyekana kuwa nchi yake inajiandaa kwenda vitani na Malawi. Kikwete alisema kuwa matamshi kuhusu vita yalitolewa na wanasiasa wa upinzani ambao wana jazba. Mjini Mzuzu mkutano uliisha bila maafikano. Siku chache baadye Rais Banda alisema kuwa mzozo huo utasuluhishwa katika mahakama ya kimataifa ya ICJ. Malawi baadaye ilikosa kufika kwenye mkutano kati yake na Tanzania kati ya tarehe 10 na 15 Oktoba kulingana na mtandao wa The Citizen

Ziwa Malawi


Je Juhudi za kidipmomasia zimefanikiwa?


Hapana. Mwanzo Tanzania imepandisha mzozo huo kwenye daraja ya juu zaidi kwa kutoa ramani mpya inayoonyesha mpaka ulio katikati mwa ziwa Nyasa. Afisaa mmoja kutoka wizara ya nyumba wa Tanzania amesema kuwa ramani hiyo inaondoa hali ya kutoelewana kwa kuonyesha mpaka unaozozaniwa. Tarehe tatu mwezi Oktoba Rais Joyce Banda aliakhirisha mkutano kati ya nchi hizo mbili hadi Tanzania itakapojieleza kuhusu ramani hiyo. Alimtuhumu Rais Kikwete kwa kumhadaa na kwamba anapanga kulipua mitumbwi ya Malawi katika ziwa hilo. Kikwete alitangaza siku hiyo hiyo kuwa Tanzania itawasilisha kesi yake katika mahakama ya kimataifa ya mizozo. Kwa upande wake Rais Banda ameutaka muungano wa Afrika kuingilia kati mozo huo. Je mzozo huu ni kuhusu mpaka tu au kuna jengine?


Sunday, October 21, 2012


Duru za jeshi la Guinea Bissau, Afrika Magharibi, zinaeleza kuwa watu waliokuwa na silaha wameuwawa kwenye shambulio dhidi ya kambi ya jeshi nje ya mji mkuu, Bissau.


Inaarifiwa mapambano yaliendelea kwa saa nzima. Waandishi wa habari wanasema shambulio hilo lilofanywa usiku wa manane, litazidisha wasiwasi Guinea Bissau, ambako jeshi lilipindua serikali mwezi wa Aprili. Fujo za mara-kwa-mara nchini Guinea Bissau zimeifanya nchi hiyo kuwa pahala pa kupitisha magendo ya mihadarati, baina ya Amerika Kusini na Ulaya.


Serikali imekataa kuongeza muda wa kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara za Mkoa wa Kagera zinazojengwa kwa kiwango cha lami na Makampuni mbalimbali kutoka nchini China zenye urefu wa zaidi ya kilomita 214 miradi ambayo kwa pamoja ina gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 250.