Friday, September 16, 2016

NUFAIKA NA BENK ZA TANZANIA

http://crdbbank.com/

Thursday, September 15, 2016

FUNITURE Warehouse Ltd

DISCOUNT KABAMBEE.!!

BET-Africa

Do your friends like your partner? Steph tries to get Kamie and Kevin to hash things out but things get out of hand when Eny intervenes. Catch the  #FinFabulous drama tonight @ 21:50 CAT.

KUMSAIDIA MKEO KAZI ZA NYUMBANI JE NIKUKALIWA AU NI MAPENZ YA DHATI?

Coca-cola

BREAKING NEWS: Trey Songz ategemewa kupiga show Coke Studio Africa October hii! Vionjo vyote vya msimu wa nne wa Coke Studio Africa hivi hapa http://spr.ly/6187BAstU

Whitedent Tanzania

Gari letu la maonesho  wiki hii litakua maeneo yafuatayo. Tafadhali ungana nasi kwa kwenda kujaza fomu katika sehemu hizi husika ili uweze kuwa mmoja wa mshindi wa magari 25 kutoka whitedent. Karibu sana!

Gari no 1 Kinondoni 1 - Mtaa: manzese daraja
Gari no 2 Kinondoni 2 - Mtaa : Ubungo River side
Gari no 4 Ilala               - Mtaa : Buguruni Sheli
Gari no 7 Arusha          - Mtaa :Kirombelo bus stand
Gari no 10 Zanzibar     - Mtaa : Mkunazini Unguja
Gari no 12 Mbeya         - Mtaa : kabwe mbeya
Gari no 15 Songea       - Mtaa :Machine ya mpunga (manzese)
Gari no 17 Singida       - Mtaa :Msifuni Sokoni
Gari no 18 Tabora        - Mtaa :Tabora Stand Mpya
Gari no 19 kigoma       - Mtaa :Soko la mwanga
Gari no 24 Geita           - Mtaa : nyankumbu

Wakumbuka hili shairi

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI"

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake, nasisitiza, kama mnataka mali mtaipata shambani